Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) wameungana na Watanzania kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye leo amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Katika tukio hilo la kupigwa risasi kwa Lissu limeonekana kuwagusa Watanzania wengi na kulaani kitendo hicho alichofanyiwa mbunge huyo huku wengi wao wakimuombea aweze kupata afya njema.

Aidha, kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amewataka watanzania kila mmoja kwa imani yake kumuombea kiongozi huyo ili aweze kupona na kuendelea na majukumu yake.  “Tumwombee Tundu Lissu, Kila mtu aombe kwa imani yake. Mungu ampe nafuu Inshallah,”ameandika kwenye ukurasa wake.

Naye Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete (CCM) amewaomba Watanzania kuwa kuwa watulivu na kumwombea kiongozi huyo, “Mungu Baba uliyeahidi kuipenda Tanzania na Watoto wako, timiza Upendo wako. Mjalie Kaka yetu Lissu afya na uzima.amina,”ameandika Ridhiwan.

CCM walaani tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu
Yametimia: Dirisha la usajili kufungwa kabla ya EPL kuanza