Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Jukwaa la Mifumo ya Chakula linalofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, amesema kupitia tafiti kupitia kilimo, mifugo na uvuvi. Kwenye kilimo Tanzania imewekeza kwenye kujua afya ya udongo.

“Tanzania kwanza tumejua kwamba kilimo ni kujua taarifa zake. Kwa maana hiyo tumewekeza sana kwenye tafiti kupitia kilimo, mifugo na uvuvi. Kwenye kilimo tumewekeza kwenye kujua afya ya udongo. Hiyo kujua afya ya udongo tuanze na data ndio tuweze kutoa huduma nzuri,” amesema Rais Samia.

Aidha ameongeza kuwa, “Kwa kutumia ICT tunaendelea kufanya ‘registration’ (kuandikisha) wakulima, aina ya kilimo wanachofanya, eneo walilonalo na mambo mengine yanayomuhusu mkulima. Lakini pia ili mkulima aweze kutoa mavuno mazuri lazima tutoe huduma za ugani zinazoeleweka.”

#RaisSamia #KeshoBora #AGRF2023.

Serikali kuongeza uzalishaji Mbegu za Kisasa
Faili la Al-Merrikh mikononi mwa Gamondi