Afara Suleiman – Babati, Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye miradi yote ambayo itapitiwa na Mwenge wa uhuru utakaowasili Oktoba 7, 2023 Wilayani Kiteto kutoka Mkoa wa Dodoma na kukimbizwa kisha kuzimwa kuzimwa Oktoba 14, 2023.
Twange ameyasema hayo na kuongeza kuwa, Mwenge huo wa uhuru unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali katika Wilaya hiyo, hivyo ni vyema wananchi wa Babati na maeneo jirani wakajitokeza wingi Ili kuipa heshima siku hiyo ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Pendo Mangali amesema Mwenge wa Uhuru utatembelea jumla ya miradi saba yenye thamani ya shilingi Billion 2.1, ambayo miwili itafunguliwa na mingine kuwekewa jiwe la msingi.
Amesema pia kutafanyika zoezi la upandaji Miti na usafi wa Mazingira kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu ya “TUNZA MAZINGIRA OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI NA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA” na kusema Mkoa wa Manyara umepewa heshima kubwa.