Mashindano ya Kili Marathon yaliyoendelea leo, Moshi mkoani Kilimanjaro yanayohusisha nchi mbalimbali yamefana leo ambapo Mtanzania, Emmanuel Giriki amekuwa mshindi wa kwanza.
Giriki amefanikiwa kuibuka mshindi akifuta vilima kwenye mbio za Kilometa 21 (half Marathon) mapema leo asubuhi.
Aidha, kati ya maelfu ya washiriki ni wafanyakazi wa Kampuni ya DataVision International yenye ofisi zake Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambao wamezoa medali kadhaa wakiwa wamedhaminiwa na huduma ya M-Lipa.
Akizungumzia hatua hiyo, afisa habari wa kampuni hiyo katika Kili-Half Marathon, Amisa Juma ambaye pia alishinda medali, ameiambia Dar24 kuwa, “medali hizo ni matokeo ya maandalizi mazuri waliyoyafanya na kujituma kuhakikisha tunafuta vilima na kama miguu itakuwa mizito tunatumia mioyo yetu.”
“DataVision kama kampuni inayoongoza kwa huduma za TEHAMA nchini, tunaamini katika ubora na kasi. Hiki ndicho tumekionesha, maandalizi mazuri na mwisho kwa kasi tumefanikiwa kujipatia medali kadhaa,” Amisa ameiambia Dar24.
“Timu ya DataVision siku zote tunahakikisha tunafanikisha kutoa huduma bora zaidi na kujali kusaidia jamii. Kuna changamoto kama unavyofuta vilima hapa, lakini mwisho hatukati tamaa na tunafanikisha. Nichukue fursa hii pia kumpongeza mshindi wa jumla, Giriki, ameiwakilisha vizuri nchi yetu kwa kuongoza katika mbio za Kilometa 21,” aliongeza.
Rais wa DRC awatangazia uhuru wafungwa wa kisiasa
Waziri wa Habari, Dkt. Harrison Mwakyembe alihudhuria tukio hilo lilikosanya makampuni na watu binafsi na amewapongeza wote walioshiriki. Takribani watu 9000 walijiandikisha kukimbia mbio fupi na ndefu (Kilometa 21 na 42).