Msanii wa Bongo Muvi, Wema Sepetu jana ameandika waraka kwa mashabiki wake wa mitandao ya kijamii na kusema amechoka na mambo ya ulimwengu kwa kutukanwa na kusengenywa kila kukicha hivyo ameamua kuachia ngazi.

Kufuatiwa na  lawama hizo Wema Sepetu amechukua uamuzi wa kuwaambia mashabiki wake kusitisha uwepo wake katika mitando ya kijamii ili kuepuka baadhi ya lawama na matusi anazozipata kutoka mitandaoni.

Katika post yake ameaandika hivi

‘’ Ipo siku nitakufa hakuna anayeishi milele, sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni  au ndo itakuwa maskini ya Mungu  dada wa watu alikuwa hivi na vile Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema…kuna wakati mwingine natamani allah wa subhanah wata’allah anichukue tu ya dunia ni mengi  sana kuna mda namkufuru Mwenyezi Mungu na kutamani labda nisinge exist… ila acha niendelee kumtegemea yeye  kila jambo hutokea kwa sababu’’ Ameandika Wema Sepetu.

Akamalizia hivi ‘’I think I need a time off on social media… kwa mara nyingine tena siwezi tena’’ akimaanisha kuwa  anahitaji kutoka katika mitandao ya kijamii kwa muda….

Kupitia ‘caption’ hiyo inasemekana kuwa mashabiki wamelinganisha na kile ambacho Diamond amekifanya siku za karibuni kwa kutoa wimbo ambao moja kwa moja umegusa maisha aliyoyaishi pindi akiwa mpenzi wa mwanadada huyo.

Hata hivyo kuna baadhi ya tetesi zinaeleza kuwa hivi karibuni mwanadada Wema Sepetu ambaye alikua muasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, alipata misukosuko iliyompelekea yeye na mama yake kuchukua uamuzi wa kuhamia chama Pinzani Cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA).

Hivyo mwanadada Wema Sepetu amejikuta katika msongo wa mawazo kwani kila kona ya mtandao amekuwa stori ya jiji, hilo limemfanya aache kutumia mitandao ya kijamii kwa muda hadi upepo huo was kendo zake utapopita.

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 1, 2017
Mwamuzi mtanzania kuchezesha kombe la dunia 2018