Polisi jijini Paris wamemuua mtu mmoja aliyetaka kuingia katika eneo la kituo cha polisi jijini humo akiwa amevaa bomu ‘feki’ la kujitoa mhanga na kisu.

Mwanaume huyo alikuwa amebeba kipande cha karatasi chenye mchoro wa bendera ya kundi la kigaidi la Islamic States of Iraq and Syria (ISIS), na maandishi yanayoelezea kuwa wao ndio wahusika wa matukio ya kigaidi.

Muendesha mashtaka wa Paris, Francois Malins aliiambia radio ya Ufaransa, France Inter Radio kuwa ni mapema sana kueleza jina halisi na mtu huyo kwakuwa bado polisi wanaendelea na zoezi la utambuzi.

Taarifa za awali zilimtaja mtu huyo kuwa ni Sallah Ali, mzaliwa wa Casablanca, Morocco.

Chanzo: The Guardian

Picha Rasmi ya Rais Magufuli yaanza kuuzwa
Msimamizi wa Bomobomoa aanguka Ghafla Ofisini, Madaktari washindwa Kubaini Tatizo