Kikosi cha Kilimanjaro Stars leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Machakos Academy licha ya mvua zinazoendelea kunyesha katika County ya Machakos.

Kilimanjaro inajiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Rwanda utakaochezwa saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos.

Mchezo huo wa kundi A una umuhimu mkubwa kwa Kilimanjaro Stars katika harakati zake za kuitafuta tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.

Kilimanjaro Stars ina pointi moja mpaka sasa baada ya kutoka sare na Libya kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kufungwa na Zanzibar kwenye mchezo wake wa pili.

Kundi A linaongozwa na Zanzibar wenye pointi sita (6) wakifuatiwa na Uganda wenye pointi (4) wakati Libya yenyewe ina pointi (3) ikikamata nafasi ya tatu ikifuatiwa na Kilimanjaro Stars na Rwanda wenye pointi (1) kila mmoja.

Mpina amtaka mwekezaji kuondoka mara moja
Rekodi za muda wote za Tanzania bara Vs Zanzibar