Kilimo cha zao la angi kimehalalishwa kisheria katika nchi ya Zimbabwe kwa ajili ya kutumika kama dawa na kwenye mambo mengine ya kisayansi
Kwa mujibu wa Serikali kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya imesema kuwa watu binafsi na taasisi zinaweza kuanza taratibu za kupata leseni kwa ajili ya kilimo hicho.
Hata hivyo, Zimbabwe inakuwa nchi ya pili barani Afrika kuruhusu kilimo hicho baada ya Lesotho kuruhusu mnamo Septemba 2017. Nchi za Malawi na Ghana zinaangalia namna ya kuhalalisha kilimo cha zao hilo ambalo nchi nyingi zinalichukuliwa kama ni moja ya dawa za kulevya.