Takriban watu tisa wamefariki na wengine 16 wamejeruhiwa, baada ya kilipuzi kulipuka kwa bahati mbaya katika eneo la Lubwe, lililopo Wilayani Rutshuru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC.
Tukio hilo lilitokea Julai 20, 2023 ambapo Kiongozi wa Shirika la kiraia katika êneo hilo, Justin Mwangaza amesema raia wa kawaida aliokota kilipuzi hicho na kukabidhi Afisa wa usalama na ndipo kilipolipuka wakati wakijaribu kukikagua.
Amesema, watu wawili walipoteza maisha papô hapo huku wengine saba, wakifariki dunia baada ya kupata majeraha mabaya wakiwa wanapatiwa huduma huku majeruhi wengine 16 wakiendelea kupokea matibabu.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa – UN, zinasema ukosefu wa usalama Mashariki mwa DRC umesababisha watu zaidi ya Milioni 1 kuyakimbia makazi yao, huku maelfu wakipoteza maisha.