Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, inaongoza kuwa na wangonjwa wengi wenye mabusha ambapo hadi sasa wamefikia 1,500 wanao subiri kufanyiwa upasuaji.
Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTDs) ulioandaliwa na shirika la afya duniani (WHO) kwa vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani wenye lengo la kuwaongezea uelewa ili kusaidia jamii kuondokana nayo.
Kaimu mratibu wa Taifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Oscar kaitaba amesema Kilwa ndio wilaya inayoongoza nchini kuwa na wagonjwa wa Mabusha.
Amesema wagonjwa hao ni wale tu waliojitokeza hospitalini na kukubali kufanyiwa upasuaji lakini inawezekana wapo wengine zaidi ambao wanaogopa kujitokeza.
” Kilikuwa na imani za kishirikina na wengine walisema ukifanyiwa upasuaji basi utapoteza nguvu za kiume lakini baada ya wengi kufanyiwa upasuaji na kupona vizuri ndipo ongezeko hilo la watu lilivyoongezeka” amesema Kaitaba.
Amebainisha mikoa ambayo tatizo hilo lipo hasa kuwa ni Dar es salaam, Lindi, Mtwara na baadhi ya maeneo ya Tanga lakini Serikali inaendelea kutoa dawa na kuhakikisha wanafanyiwa upasuaji.
Mganga mkuu wa Serikali dkt. Mohamed Kambi amesema kama Tanzania iliamua kuchukua hatua dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele ili dunia iweze kuyapa kipaumbele.