Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ametangaza sheria mpya yenye lengo la kupambana na kudhibiti tamaduni za kigeni.

Marufuku hiyo ni Pamoja filamu za kigeni, mavazi ya kigeni na misemo ya kigeni (misimu) na yeyote atakayekikuka atakuhukumiwa kifo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa Kim anafanya juhudi kulinda utamaduni Korea ya Kaskazini usiingiliwe na tamaduni za nje hasa kupitia filamu na muziki.

Hii si mara ya kwanza kwa Korea Kaskazini kufanya hivi na Taifa hilo ni moja kati ya mataifa yenye sheria kali zaidi duniani ambayo yanajitahidi sana kujidhibiti kutokuiga tamaduni za mataifa ya Magharibi.

Kupitia tovuti ya BBC, binti Yoon Mi-so aliyewahi kuwa raia wa Korea Kaskazini anasema alikuwa na miaka 11 pekee wakati alipoona mtu wa kwanza kunyongwa kwa kukamatwa na mchezo wa kuigiza (filamu) wa Korea Kusini.

Akizungumza na BBC kutokea nyumbani kwake Seoul, ameeleza kuwa majirani zake wote waliamriwa kutazama na ikiwa mtu hakufanya hivyo, alihesabiwa kama mhaini.

Walinzi wa Korea Kaskazini walikuwa wanahakikisha kila mtu anajua adhabu ya kusafirisha video haramu ni kifo.

“Nina kumbukumbu kubwa ya mtu ambaye alikuwa amefunikwa macho, bado ninaweza kuona machozi yake yakitiririka. Hiyo ilikuwa ni kiwewe kwangu. Kifuniko cha macho kilikuwa kimelowa kabisa na machozi yake.

“Walimweka juu ya mti na wakamfunga, kisha wakampiga risasi,” amesimulia Yoon Mi-so.

Haikuwa kazi rahisi - Anjella
Maambukizi ya Corona yashika kasi Uganda, hatua kali zatangazwa