Kwa mara ya kwanza Kim Jung Un ameonekana hadharani akiwa anakata utepe kwenye uzinduzi wa kiwanda cha mbolea baada ya siku 20 ambazo hakuonekana hali iliyopelekea kusambaa kwa taarifa kuwa huenda rais huyo ameaga dunia.

Taarifa hiyo imeripotiwa na vyombo vya habari mbalimbali nchini Korea Kusini.

Shirika la habari la taifa, KCNA limeeleza kuwa Kim aliambatana na maafisa kadhaa wa Korea Kaskazini akiwemo dada yake Kim Yo Jong, jambo lililofanya watu waliokuwepo kiwandani hapo kushangilia kwa furaha.

Haya hivyo, Shirika hilo la habari halikutoa picha zozote wala kuelezea wapi alikuwa kiongozi huyo.

Naye Rais wa Marekani, Donald Trump, alipoulizwa kuhusu kuonekana kwa kiongozi huyo alijibu “Siwezi kusema chochote kwa sasa.”

Taarifa kuhusu hali mbaya ya afya ya Kim ilianza kusambaa baada ya kiongozi huyo kukosa kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo, Kim II Sung, mnamo Aprili 15, 2020.

Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo ni tukio kubwa sana katika matukio ya nchi hiyo, na Kim mara zote hutembelea alipozikwa babu yake na hajawahi kukosa tukio hilo hapo kabla.

Serikali yasambaza vifaa kinga kwa watumishi wa afya
WHO yatarajia mwaliko China kuchunguza chimbuko la Corona