Rais wa Marekani, Donald Trump na mshauri wake wa usalama wa taifa wametofautiana juu ya uzito wa tishio la Korea Kaskazini lililopo sasa hivi.

Katika ujumbe wa Tweeter aliotuma kutoka Tokyo, Trump amemjibu, John Bolton ambaye siku moja iliyopita aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakuna shaka kitendo cha Korea Kaskazini kujaribu kombora la Balistika la masafa mafupi limevunja azimio la Umoja wa Mataifa.

Kauli ya Bolton ni ya kwanza kutolewa na afisa wa Marekani akieleza kuwa kitendo cha Korea Kaskazini kurusha kombora ni kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa.

“Korea Kaskazini ilifyatua baadhi ya silaha hizo ndogo ambazo zimewakera baadhi ya watu wangu na wengine, lakini sio mimi mwenyewe,” Trump amesema katika ujumbe wake wa tweeter.

Lakini baadhi ya wachambuzi wanaeleza kuwa kurushwa kwa makombora hayo ni suala lenye kuleta wasiwasi.

“Ni dhahiri kuwa kurushwa kwa kombora kunakiuka vikwazo vilivyowekwa na UN, haijalishi ni la umbali gani, Ukweli ni kuwa majeshi ya Marekani na raia nchini Korea Kusini na Japan tayari wako katika umbali ambao makombora ya Korea Kaskazini yanaweza kuwafikia, na hivyo basi kukubali makombora ya masafa mafupi au ya kati kunaiweka Marekani hatarini, na hivyo hivyo washirika wetu Japan na Korea Kusini,” Kevin Maher, mshauri wa mambo ya usalama Washington na mkuu mstaafu wa Kitengo cha Masuala ya Japan katika Wizara ya Mambo ya Nje

Katika taarifa hiyo, siyo Kim aliyetoa maneno ya kashfa kuhusu makamu wa rais wa nchi hiyo, Joe Biden, bali ni maoni yaliyokuwa hayana jina yaliyochapishwa na shirika la habari kuu la Korea Kaskazini, ambayo yalimuelezea mwanasiasa wa Marekani kuwa ni “mpumbavu mwenye ufahamu mdogo” na mtu mpuuzi mwenye viwango vya chini kama binadamu.”

Hata hivyo, Trump katika ujumbe wake wa Tweeter kuwa Kim anajaribu kumtumia ishara akimaanisha kuwa kiongozi wa Pyongyang anapendelea kufanya mazungumzo na rais wa hivi sasa wa Marekani na siyo mgombea wa chama cha upinzani.

Video: Mwanamke mwenye misuli zaidi duniani
Vyama vikubwa vyapata pigo barani Ulaya