Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong un amemualika rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in kufanya ziara katika mji mkuu wa nchi Pyongyang kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
Mwaliko umekuwa ni wa kwanza baada ya kupita muongo mmoja kukutana kwa marais wa nchi hizo ambazo zimekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu.
Aidha, Rais Moon amesema kuwa mkutano huo na Korea Kaskazini ni wa muhimu, huku akiitaka Korea Kaskazini kurudi katika meza ya mazungumzo na Marekani.
Mualiko huo ulikabidhiwa kwa rais wa Korea Kusini na dada yake rais Kim Jong un , Kim Yo Jong alipohudhuria ufunguzi wa michezo ya Olympic inayofanyika Korea Kusini.
Hata hivyo, Makamu rais wa Marekani, Mike Pence alisusia mwaliko wa chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.