Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Jong-un ameomba msamaha kufuatia mauaji ya afisa wamajirani zao Korea Kusini.

Taarifa toka ofisi ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in inasema raisi Kim jong-un ameripotiwa kumwambia mwenzake wa Korea Kusini kwamba tukio hilo halikustahili kufanyika.

Korea Kusini inadai mtu huyo mwenye umri wa miaka 47-alikuwa akijaribu kutoroka kutoka Korea Kaskazini alipopatikana na wanajeshi wa nchi hiyo walikuwa wakifanya doria, Baada ya hapo alipigwa risasi na mwili wake kuteketezwa moto.

Msamaha huo ulitolewa kupitia njia ya barua iliyotumiwa Rais Moon kuelezea kuwa tukio hilo halikustahili kufanyika.

kwa mujibu wa taarifa hiyo . Bw.Kim alisema “naomba msamaha” kwa “kuwakosea” Bw Moon, imeripotiwa na shirika la habari la Yonhap, likinukuu Blue House.

Korea Kaskazini imetolea maelezo zaidi kuhusu tukio hilo, ikisema mtu huyo alipigwa risasi kumi na kufafanua haikuchoma mwili wa mtu huyo bali ni “kifaa kilichokuwa kinaolea majini” ambacho kilitumia kumbeba, mkurugenzi wa usalama wakitaifa wa Kusini Suh Hoon.

Shibuda :NEC anzisheni tume ya upelelezi
Sven: Ni pigo kumkosa Fraga

Comments

comments