Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un anatarajia kukutana na Rais wa Korea Kusini kufanya mkutano mwezi ujao, kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa nchi hizo mbili.
Mkutano huo utakuwa wa kwanza tangu, Kim Jong-un aingie madarakani hivyo unalenga kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliozigubika nchi hizo.
Aidha, kwa mujibu wa ujumbe wa Korea Kusini uliokutana na Rais huyo, umesema kuwa, Kim amesema kuwa angependa kuzungumzia masuala ya kuachana na silaha za nyuklia ikiwa tu atahakikishiwa usalama wa nchi yake.
Hata hivyo, Kim na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in watakutana kwenye mpaka wenye ulinzia mkali mwezi ujao katika kijiji cha mapatano cha Panmunjom, ambapo pia watazungumzia kuhusu kufungua mawasiliano ya simu kati ya viongozi hao.