Rais wa korea kaskazini Kim joung-un ametuma mualiko kwa Papa kwenda nchini kwao.
Mualiko huo utawasilishwa rasmi na Rais wa Korea kusini Moon Jae-in, ambaye anatarajia kwenda Vatcan mwezi ujao kama moja ya ziara yake nchini Uingereza.
Kihistoria hakuna Papa aliyewahi kutembelea nchi ya Korea Kaskazini japokuwa marehemu Papa John Paul II aliwahi kualikwa mwaka 2000.
Katika mualiko huo ambao ulitolewa na baba yake Kim joung-un, licha ya kutoweza kufanikiwa papa John alinukuliwa akisema itakuwa ni muujiza kama akienda korea.
Na mualiko wa mwaka huu utawasilishwa baada ya kikao kati ya Papa Francis na Rais wa Korea kusini.
Ikumbukwe kuwa rais Kim mwaka huu amefenikiwa kukutana na Rais wa Marekeni Donald Trump jambo ambalo lilishangaza watu wengi.
Nchi ya korea kaskazini haina mahusiano mazuri ya kidiplomasia na Vatcan, kwani waumini wa dini ya katoliki hawashilikishwi na uongozi wa juu wa dini hiyo uliopo Vatcan.