Kanye West ameweka wazi kuwa anajaribu kumrudisha mke wake Hata hivyo, bado inaonekana Kim Kardashian anaweza kuwa na mipango mbadala linapokuja suala la hali ya
mahusiano kati yake na Ye.

Kwa mujibu wa TMZ, Kim bado anasonga mbele linapokuja suala la kuachana na Kanye, na ili mchakato uende haraka zaidi, inasemekana amefungua kesi ya kudai kuachana
kihalali.

Nyaraka hizo ziliripotiwa kuwasilishwa Ijumaa Nov 10, 2021, Kim anamwomba jaji kutenganisha masuala ya malezi ya watoto na mali na hali yao ya ndoa. Pia anaomba jina lake la ukoo lirejeshwe, kumaanisha kuwa haitaji tena kuitwa “West” kufuatia hali halisi ya kimahusiano waliyonayo.

Habari hizi zinakuja saa chache baada ya Kanye kubadilisha mashairi kwenye wimbo wake “Runaway,” ambapo alisema, “Run back to me”   hasa zaidi kauli hiyo ilileta maana ya kumtaka Kim amrudie pale alipomtaja Kim kwa jina lake halisi, ‘Kimberly’.

Licha ya kelele zote ambazo Kanye amekuwa akizipiga ili kumrudi Kim kwenye maisha yake ila bado kwa sasa inaonekana kama Kim amechagua zaidi kusonga mbele na sio kurudi nyuma.

Arudisha milioni kumi alizookota
Wanandoa watupwa Jela miaka 20 kwa kosa la kumtesa mtoto wao.