Kim Kardashian anaendelea kujikita katika kuhakikisha anavaa taji la malikia wa ‘selfie’ duniani kwa jinsi anavyoonesha kuchanganyikiwa na picha za aina hiyo hata pale anapokutana na watu anaowakubali zaidi duniani.

Mapema Jana asubuhi, Kim Kardashian na Kanye West waliripotiwa kuwa watashiriki tukio la kuchangia fedha lilitayarishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani, Bi. Hillary Clinton, jijini Los Angeles. Dakika chache baadae Kim Kardashian alipost kwenye Instagram kuelezea kiu yake ya kupata selfie na Hillary Clinton.

Usiku wa tukio hilo, Kim Kardashian na mumewe Kanye West walifanikiwa kupoz na kuselfika na mwanasiasa huyo mkongwe ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton.

Kim K aliandika caption akimpigia debe Bi. Hillary anaepanga kuwania nafasi ya urais wa Marekani katika uchaguzi ujao.

“I got my selfie!!! I really loved hearing her speak & hearing her goals for our country! #HillaryForPresisent,” aliandika.

I got my selfie!!! I really loved hearing her speak & hearing her goals for our country! #HillaryForPresident

A photo posted by Kim Kardashian West (@kimkardashian) on

Kim Kardashian ni mpenda Selfie haswa, na aliwahi kutayarisha kitabu chake cha ‘selfie’.

 

Picha: Diamond Na Zari Wapata Mtoto wa Kike
CUF Wajipanga Kumjibu Ibrahim Lipumba, ‘Tumepitia Mengi’