Siku hizi imekuwa fasheni wasanii wengi wa nje ya nchi kutunga mimba na kubebesha mimba hiyo mtu mwingine, ni kutokana na sababu mbalimbali za kiafya ikiwemo mwanamke kushindwa kutunza mimba hiyo au sababu nyingine ambazo hazijafahamika.

Kanye West na Kim Kardashian hivi karibuni wanatarajia kupata mototo wao wa tatu, mtoto huyo hatolelewa katika tumbo la uzazi la mwanadada, mlimbwende Kim kardashian.

Kutokana na sababu ambazo daktari wameeleza, kuwa Kim kardashian hana uwezo wa kubeba mimba na endapo ikatokea amebeba mimba hali hiyo inaweza kumsababishia kifo.

Hivyo mwanadada aliyekubali kubeba mimba hiyo amepewa masharti makali yaliyopelekea kumlipa gharama kubwa ambapo amelipwa kiasi cha fedha dola 45000 yenye thamani ya Tsh1000,890,000 kwa pesa za kitanzania.

Fedha hiyo imelipwa ili kuhakikisha dada huyo yupo katika hali ya usalama kwa matunzo ya mototo wao anayetarajiwa kuzaliwa hivi karibuni.

Hata hivyo mwanadada huyo amepewa onyo kufanya mambo ambayo yatahatarisha maisha ya mototo ikiwemo kuvuta sigara, kunywa pombe, kutumia dawa za kulevya, kuoga kwenye maji moto sana na pia ametakiwa kula vizuri ili kumfanya mtoto aweze kukua katika ukamilifu.

Taarifa hizo zimetolewa na Tovuti ya Habari za burudani nchini Marekani ya TMZ.

Ripoti ya Tanzanite, Almas yawatafuna Mawaziri
Spika Ndugai alivyopokea ripoti ya kamati maalumu za kuchunguza Tanzanite, Almasi