Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ‘TAIFA STARS’ Kim Poulsen amekiri kuridhishwa na maendeleo ya kikosi chake kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa kufuzu Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ dhidi ya Somalia.

Stars itacheza Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (Julai 23) Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa mwenyeji, huku mchezo wa Mkondo wa Pili ukipangwa kufanyika Uwanja huo huo (Julai 30).

Kocha Kim amesema hadi sasa wachezaji wote aliowaita kambini wanaendelea vizuri na anaamini watafanya vyema katika mchezo dhidi ya Somalia, ambao amekiri utakua na changamoto za kiushindani kutokana na wapinzani wao kuimarika siku hadi siku.

“Kila mchezaji anaendelea vizuri tangu tulipoanza kambi, nina uhakika mchezo wetu dhidi ya Somalia utakua na upinzani mkubwa, hivyo maandalizi yetu yamezingatia hilo kutokana na kutambua umuhimu wa kushinda mchezo, ili tuweze kusonga mbele.” amesema Kocha Pulsen

Taifa Stars Jana Jumanne (Julai 19) ilicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Sudan jijini Dar es salaam na kupata matokeo ta sare ya 1-1, hatua ambayo imeonyesha kumfurahisha Kocha Kim Poulsen kufuatia kuwaona wachezaji wake wakipambana kwa kufuata maelekezo anayoendelea kuwapa katika kipindi hiki cha maandalizi.

Simba SC yaahidi kurudisha furaha 2022/23
Mabingwa wa Uganda wahusishwa Siku ya Wananchi