Baada ya Timu Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kushindwa kufuzu hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 ukanda wa Bara la Afrika, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulen amesema kukosa uzoefu kwa wachezaji wake ndio sababu ya kushindwa kufikia lengo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio wameibuka vinara wa Kundi J wakikusanya alama 11, wakifuatiwa na Benin waliomaliza nafasi ya pili kwa kufikisha alama 10, huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 8 na Madagascar ya mwisho katika kundi hilo kwa kuwa na alama 4.

Poulsen amewapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa na ngumu waliyoifanya hadi kumaliza nafasi hiyo waliyoishia.

“Kilichotugarimu ni kukosa wachezaji wenye uzoefu kama ilivyo kwa wenzetu Congo, Benin na Madagascar lakini lazima niwapongeze wachezaji wangu wamefanya kazi nzuri,” amesema Poulsen.

Amesema katika kundi lao la J, ni Tanzania pekee ambayo kwenye kikosi chake ilikuwa na idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza ligi ya ndani tofauti na wapinzani wao ambao asilimia 80 walitumia wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi zao.

Wachezaji wa Tanzania ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya Tanzania ni Novatus Disman anayechezea Mekab Tel Aviv, Simon Msuva Wydad Casablanca ya Morocco na nahodha Mbwana Samatta anayekipiga Antipways ya Ubelgiji.

Poulsen amesema pamoja kukosa nafasi hiyo, lakini anaamini miaka michache ijayo Tanzania itashikiri mashindano makubwa duniani na hiyo ni kutokana na mchezo huo kukua kwa kasi nchini.

Kocha huyo pia amewataka wachezaji wa Tanzania kuongeza juhudi ili kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 17, 2021
Flaviana Matata afichua siri za magumu aliyopitia baada ya ndoa yake kuvunjika