Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen, amesema bado kuna kazi kubwa ya kuisuka vyema safu yake ya ulinzi.

Stars ilishinda mchezo huo wa Kimataifa wa Kirafiki Jumatano (Machi 23), Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michezo ya kusaka nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ na Fainali za Mataifa Bingwa barani humo ‘CHAN 2024’.

Kocha Kim amesema safu yake ya ulinzi kuna muda imekua inajisahau na kufanya makosa yanayoweza kurekebishika, hivyo ni jukumu lake na Benchi la Ufundi la ‘Taifa Stars’, kulifanyia kazi tatizo hilo kabla ya kuanza Mshike Mshike wa kusaka nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ na Fainali za Mataifa Bingwa barani humo ‘CHAN 2024’

“Bado tuna kazi kubwa kwenye safu ya ulinzi kwa sababu kuna muda wanajisahau na kupoteza umakini, hili jambo nafikiria sio zuri hasa unapokutana na mpinzani mzuri.”

“Nina imani mchanganyiko wa wachezaji utasaidia kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yetu ikiwemo AFCON na CHAN.” Amesema Kocha huyo kutoka nchini Denmark

Taifa Stars itacheza Mchezo mwingine wa Kimataifa wa Kirafiki Jumanne (Machi 29) dhidi ya Timu ya Taifa ya Sudani, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC yaomba mashabiki 10,000 CAF
Manara: Wananchi msiyumbishwe na maneno ya mitandaoni