Baada ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2019/20 kuzinduliwa rasmi kwa matokeo ya kustaajabisha, mashabiki wa soka duniani leo wataendelea na burudani ya soka, kwa kuanza kushuhudia mtanange wa michuano ya Europa League hatua ya makundi.
Michuano hiyo ambayo ni ya daraja la pili kwa ubora upande wa vilabu barani humo, itarindima kwa timu 64 zilizopangwa kwenye makundi 12 kupambana vilivyo, huku kila timu ikizihitaji alama tatu za kuanzia safari ya kulitafuta taji la michuano hiyo.
Katika michuano hii, England inawakilishwa na klabu za Arsenal na Man Utd, Hispania (Getafe na sevilla), Italia (SS Lazio na AS Roma), Ujerumani (Borussia Mönchengladbach na VfL Wolfsburg), ambazo zitapambana na klabu za mataifa mengine ya bara la Ulaya.
Michezo ya michuano hiyo hatua ya makundi inayoanza rasmi hii leo.
Kundi A
APOEL Nicosia Vs F91 Dudelange
Qarabag FK Vs Sevilla
Kundi B
Dynamo Kyiv Vs Malmoe FF
FC Koebenha Vs nvLugano
Kundi C
FC Basel Vs FC Krasnodar
Getafe Vs Trabzonspor
Kundi D
LASK Vs Rosenborg
PSV Eindhoven Vs Sporting CP
Kundi E
CFR Cluj Vs Lazio
Rennes Vs Celtic
Kundi F
Eintracht Frankfurt Vs Arsenal
Standard Liege Vs Vitoria de Guimaraes
Kundi G
FC Porto Vs Young Boys
Rangers Vs Feyenoord
Kundi H
Espanyol Vs Ferencvaros
Ludogorets Razgrad Vs CSKA Moscow
Kundi I
Gent Vs Saint-Etienne
Wolfsburg Vs FC Olexandria
Kundi J
Borussia Moenchengladbach Vs Wolfsberger AC
AS Roma Vs Istanbul Basaksehir
Kundi K
Slovan Bratislava Vs Besiktas
Wolverhampton Wanderers Vs Braga
Kundi L
Manchester United Vs FC Astana
Partizan Beograd Vs AZ Alkmaar