Kasi ya kufuta ubadhirifu serikali imewakumba maafisa wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) ambapo shirika hilo limewafukuza kazi maafisa wake saba na kuwafikisha wengine mahakamani.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa maafisa hao wamefukuzwa kazi kutokana na kujihusisha na vitendo vya wizi na ubadhirifu.

Alisema kuwa mafisa hao saba walikuwa wanafanya kazi katika mikoa ya Kagera, Dodoma (Kondoa Kaskazini), Shinyanga, Katavi pamoja na mkoa wa Tanesco wa Ilala.

Mramba alieleza kuwa maafisa ambao tayari wameshafikishwa mahakamani ni wale wa mkoa Kagera.

“Wale maofisa wa mkoa wa Kagera wiki iliyopita walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili,” alisema.

“Huu ni mwanzo, tumedhamiria kupambana na wafanyakazi wasiokuwa waadilifu ndani ya shirika,” Mramba aliongeza.

TRA Yaishukia Bakwata, Yaipa Siku Saba Kuwasilisha Nyaraka
Chris Brown Amzawadia Gari La Kifahari Mwanamke Aliyenyanyaswa