Kimbunga keneth Kimetua kaskazini mwa Msumbiji na kufanya uharibifu huku bado nchi hiyo inatarajia kukumbwa na dhoruba nyingine kubwa.
Licha ya kuwa saa chache zilizo pita kimbunga hicho kilikuwa kimepungua kasi, utabili wa hali ya hewa wa nchi hiyo unategemea kuwa kutakuwa na mvua kubwa ambayo itasababisha mafuriko.
Idara ya kudhibiti majanga nchini Msumbiji imesema watu elfu thelethini wamehamishwa katika makazi yao ambapo dhoruba ya kimbunga inaweza kupiga tena.
Kimbunga hicho chenye nguvu kilikuwa na upepo wenye kasi ya kilometa 220 kwa saa baada ya kupata nguvu katikati ya wiki hii na kuwa sawa na tufani ya awamu ya nne katika bahari ya Atlatic mashariki mwa bahari ya Pacifiki kabla ya kuwasili.
Kabla ya kupiga nchi ya Msumbiji kimbunga Keneth kiliwaua watu watatu katika taifa la kisiwani la Comoros siku jumatano usiku.