Watu wanaoishi kusini mashariki nchini Marekani wametakiwa kuondoka haraka katika makazi yao ili kukipisha kimbunga Michael ambacho kinakaribia kulikumba eneo hilo.

Taarifa za watabiri wa hali ya hewa zimesema kuwa kimbunga hicho kwa sasa kimeingia katika hatua ya tatu na kuongezeka kasi yake kwa kadri kinavyopitia ghuba ya Mexico kuelekea Majimbo ya Florida, Alabama na Georgia.

Aidha, Kimbunga hicho kinakwenda kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa, ambapo wataalam wamesema kuwa wakazi wa jimbo la Florida leo huenda watakumbwa na mawimbi ya maji yatakayo sababishwa na upepo huo hatari, hivyo wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kuondoka maeneo yanayolengwa na kimbunga Michael.

Kwa upande wake, Gavana wa jimbo la Florida, Rick Scott ametoa tahadhari kubwa kwa wakazi wa jimbo hilo ambapo amesema kuwa kimbunga hicho ni hatari zaidi.

Kutokana na hali hiyo majimbo ya Alabama, Florida na Georgia yametangaza hali ya hatari, ambapo Alabama maeneo 92 ya watu wake wanatakiwa kupisha madhara ya kimbunga hicho Michael kusini mwa jimbo la Georgia na maeneo 35 ya jimbo la Georgia kimbuka hicho kinatarajiwa kuyafikia.

Naye Gavana wa Jimbo la Carolina Kaskazini, Roy Cooper ameonya kwamba watu wake wanatakiwa kuchukua tahadhari kwani huenda madhara ya kimbunga hicho yakawa makubwa zaidi ya Kimbunga Florence kilicholikumba eneo hilo mwezi uliopita.

 

Majaliwa akerwa na biashara ya magendo
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 10, 2018