Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh amemfukuza kwenya kambi ya timu nchini Ubelgiji, kipa na Nahodha Vincent Enyeama baada ya kuchelewa kuingia kambini.

Kipa huyo namba moja wa Lille ya Ufaransa, inaelezwa alibishana na kocha, kwa kuendelea kueleza sababu za kuchelewa kwake licha ya kuambiwa anyamaze na kuondoka.

Na kipa huyo alipogoma kuondoka, kocha huyo aliwaita walinzi waje kumfukuza. Pamoja na Enyeama kutaka kujitetea, lakini hakupata fursa hiyo kwa Oliseh.

Sakata hili linaibuka baada ya kipa huyo kurejea kambini akitoka kwenye mazishi ya mama yake.

Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) limethibitisha mtafaruku baina ya wawili hao, lakini wakajaribu ‘kupoza poza’. “Ni kweli kulikuwa kuna kutoelewana kidogo kambini, lakini tatizo hilo limetatuliwa na Enyeama amebaki kambini”.

Timu ya taifa ya Nigeria hii leo itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya jamuhuri ya Kidemokrasia Ya Kongo.

Ademi Alitumia Dawa Za Kusisimua Misuli
Lowassa: Nimewaona CCM WakipitaPita Monduli…