Kinara mkuu wa biashara haramu ya madawa ya kulevya wa kikundi cha Beltrán Leyva ametiwa mbaroni baada ya kukamatwa na majeshi ya Mexico.

Kiongozi huyo mkuu anayefahamika kwa jina la Eleazar Palomo Castillo (El Cochi au The Pig) amekamatwa baada ya kukataa kusimamisha gari yake katika kizuizi cha ukaguzi karibu na uwanja wa ndege wa Monterrey, Mexico.

kwa mujibu wa Jeshi la Mexico, El Cochi au The Pig, anatajwa kuwa kama kiongozi mkuu wa madawa ya kulevya katika mji wa San Pedro Garza García, na naibu kamanda wa kundi hilo katika jimbo hilo linalo pakana na Marekani.

 

Mpoto aunga mkono mapambano madawa ya kulevya, ampongeza Makonda
Mahakama yapingana vikali na Trump, yakataa rufaa