Barcelona imeamua kuingia kwenye vita ya kumnasa Mcameroon, Breel Embolo.

Embolo ndiyo ana miaka 18 tu na anaendelea kuwa nyota katika kikosi za Basel ya Uswiss.

Mcameroon huyo sasa ana uraia wa Uswiss na amekuwa tishio katika ligi ya nchi hiyo hadi Ligi ya Mabingwa.

Barcelona imeeleza wazi kuingia kwenye vita hiyo licha ya kujua timu nyingine kama Juventus, Arsenal na Manchester, nazo zimeingia kwenye vita ya kumnasa.

Kocha Wa Yanga Afanya Maamuzi Magumu
Simba Yaiongeza Nguvu Kwenye Safu Ya Ulinzi