Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amemjibu mhadhiri wa Chuo Kikuu, Dkt. Benson Bana aliyeukosoa uamuzi wa mwanasiasa huyo mkongwe wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokitumikia kwa zaidi ya nusu karne akianza na Tanu.

Akiongea katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa uliofanyika jana mjini Geita, Kingunge alisema kuwa Dkt. Bana alitoa maoni yake bila kufanya utafiti na kuifahamu historia yake ndio sababu alisema yeye (Kingunge) huwa hafanyi maamuzi yake bali anafanyiwa maamuzi na Lowassa.

Mzee huyo alitumia maneno makali juu ya msomi huyo ambaye ni kada wa CCM, akidai kuwa ingawa alisomeshwa vizuri, ana ugonjwa wa ‘uvivu wa kufikiri’.

“Vijana tunawasomesha vizuri, lakini wanashindwa kutumia akili zao. Wanaugonjwa ambao Mwalimu aliuita ‘intellectual laziness’, yaani ‘uvuvi wa kufikiri’. Kwa sababu wasomi hawa wanatakiwa wasiseme mambo bila kufanya utafiti. Dkt. Bana hanijui vizuri, hasomi historia yangu. Anakurupuka tu kwamba eti mimi huwa sifanyi maamuzi yangu ila nafanya maamuzi ya ndugu Lowassa. Angekuwa amefanya utafiti asingeweza kusema hayo.”

Mzee Kingunge alitangaza rasmi kuachana na CCM akidai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo na kimevunja katiba yake baada ya kwenda kinyume cha taratibu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wake wa urais.

 

Profesa Kitila Auponda Mdahalo Wa Taasisi Ya Mwalimu Nyerere
Balozi Juma Mwapachu aitosa CCM