Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kingwangalla amekabidhi magari 6 kwa Halmashauri 6 na kuyataka yatumike katika kukabiliana na ujangiri nchini.
Ambapo wabunge wamekabidhiwa magari hayo leo katika ofisi za makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
Wabunge waliokabidhiwa ni kutoka Bunda Vijijini, Boniface Getere, Mbunge wa Itilima, Njalu Silanga, Mbunge wa Longido, Dk. Steven Kiruswa, Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay na Mbunge wa Tanganyika, Moshi Kakoso.
”Tunakabidhi magari amabapo Halmasahauri 6 zitanufaika ambayo yanatokana na jitihada za waheshimiwa wabunge kutusumbua sana lakini pia utashi wao kuunga mkono katika vita dhidi ya ujangili” amesema Kingwangalla.
-
Mbunge CUF alituhumu jeshi la Polisi
-
Magazeti ya Tanzania leo Mei 13, 2018
-
Korea Kaskazini yatangaza uamuzi mzito kwa silaha zake za nyuklia
Ameongezea kuwa magari hayo yatasaidia katika kufanya doria usiku lakini pia kuitikia kwa haraka pale panapotokea kesi za wanyama waharibifu mfano katika maeneo ya Bunda vijijini ambako kumekuwa na mwingiliano wa wanyama pori.
Aidha mbali na hilo amesema kuwa Serikali ina mpango wa kujenga madungu kwa ajili ya kuangalia wanyama kwa mbali wakiwa ndani ya hifadhi lengo likiwa ni kuhakikisha maeneo yote kuzunguka mbuga ni salama dhidi ya ujangili wa wanyama.