Watu 11 wamekamatwa kwa kosa la kumkamata Meya wa Las Margaritas katika Jimbo la Chiapas, Jorge Luis Escandón Hernández kisha kumfunga katika gari na kumburuza katika mitaa mbalimbali.
Ambapo Polisi waliingilia kati tukio hilo na kumuondoa meya Jorge Luis Escandón Hernández ambae alipatwa na majeraha kidogo.
Hili ni shambulio la pili kutoka kwa wakulima hao ambao wanadai wameamua kufanya hivyo mara baada ya meya huyo kutotimiza ahadi zake alizotoa kwa wananchi hao ikiwemo ujenzi wa barabara.
Meya pamoja na viongozi wa chini wa Serikali mara nyingi hushambuliwa nchini Mexico na makundi ya kihalifu wasipofanya matakwa wanayoyataka, lakini kupigwa kutokana na ahadi za uchaguzi ni jambo geni.
Aidha mitandaoni kumesambaa video zilizochukuliwa na wapita njia nje ya ofisi ya Meya huyo na kusambaa mtandaoni zimeonesha kundi la Wanaume wakimvuta nje ya jengo na kumfunga nyuma ya gari na kumburuza katika mitaa ya Santa Rita
Baada ya Meya Hernández kufanyiwa tukio hilo amesema atafungua kesi ya kutekwa na kutaka kuuwawa, itakumbukwa kuwa miezi kadhaa iliyopita watu wasiojulikana walivamia na kuharibu ofisi yake, lakini yeye hakuwepo.