Naibu mwenyekiti wa kampuni ya Samsung Lee Jae-Yong na Rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Gue-hye waadhibiwa vikali kwa kufanya ufisadi mkubwa wa kuilaghai serikali na kuitaka iunge mkono mabadiliko ndani ya kampuni ya Sumsang.

Ambapo waendesha mashtaka nchini Korea walifungua kesi ya ufisadi na kutaka aliyekuwa naibu mwenyekiti wa kampuni ya Samsung, Lee Jae-Yong kufungwa jela miaka 12.

Kupitia kesi hiyo aliyekuwa rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Gue-hye ameondolewa madarakani kwa kukiuka sheria na kujihusisha na ufisadi.

Inasemekana kuwa viongozi hao walitumia pesa nyingi sana kumhonga mshirika wa karibu wa Rais Park, Choi Soon-sil ili wapate kupendelewa na Rais.

Pamoja na hayo yote Lee amekanusha tuhuma hiyo na kupelekea kesi yake kusogezwa mbele ili kuruhusu chunguzi uweze kufanywa zaidi, hukumu yake inatarajiwa kutolewa tarehe 27, mwezi huu.

 

Arsenal FC Wamnyatia Lucas Moura
Kaburu, Aveva Warudishwa Rumande