Kiongozi wa Mpito Nchini, Mali Assimi Goïta amenusurika kuchomwa kisu na wanaume wawili wakati alipohudhuria ibada ya ya siku ya Eid ul-Adha katika msikiti wa Grand Mosque. katika msikiti uliopo mji mkuu, Bamako.

Ka mujibu wa Shirika la Habari la AFP, mafisa wanasema washambuliaji, walikuwa ni wawili, wamekamatwa na rais ameondolewa kwenye msikiti huo kwa usalama wake.

Kabla ya mapinduzi ya mwezi Agosti nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na maadamano juu ya ufisadi na waasi wa Kiislam walikuwa wameyateka maeneo mengi ya nchi.

Kanali Goïta aliingilia kati tena mwezi Mei, akachukua nafasi ya serikali ya mpito na kuchukua mamlaka kama rais- aliahidi kukabidhi utawala wa kiraia mamlaka kama ilivyopangwa mwaka ujao.

TFF yakiri kudaiwa Milioni 76
Finland yaipongeza Tanzania kwa uhuru wa habari, utawala bora