Chama cha Upinzani kilichopigwa marufuku cha Patriots cha nchini Senegal, kimesema Kiongozi wao, Ousmane Sonko, ambaye amekuwa akigoma kula wakati akiwa gerezani kama njia mojawapo ya kulalamikia mashitaka ya jinai dhidi yake.
Sonko alipelekwa jela wiki iliyopita, kabla ya kesi yake kusikilizwa akituhumiwa kuitisha mapinduzi dhidi ya Serikali huku sababu za kulazwa kwake zikiwa hazijawekwa wazi, ingawa alikuwa na afya njema kabla ya kuwekwa jela.
Julai 30, 2023 kupitia ukurasa wake wa Twitter, Sonko alisema angeanza kususia chakula na kulazwa kwake kunakuja ikiwa ni siku moja kabla ya jaji wa Mahakama ya Dakar, kuamuru apelekwe jela.
Hata hivyo, mashitaka ya hivi karibuni dhidi ya Sonko yamekuja wiki chache baada ya Mahakama kumpata na hatia ya kuchochea vijana na kupewa hukumu ya miaka 2 jela, hatua iliyosababisha maandamano makubwa kote nchini Senegal.