Kiongozi wa Kitaifa wa chama kikuu cha upinzani cha Cameroon, Ni John Fru Ndii ametangaza kutowania tena nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2018.
Ndii ambaye alianzisha chama cha upinzani chenye nguvu zaidi nchini humo cha Social Democratic Front (SDF) mwaka 1990 amekuwa akigombea nafasi hiyo na kuleta ushindani mkali.
Akizungumza katika mkutano wa chama hicho uliofanyika Bamenda, Ndii mwenye umri wa miaka 77 amesema kuwa ameamua kuwaachia nafasi kizazi kipya katika siasa alichokipika.
“Sitagombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu. Nataka mchague nani atakayekuwa bora zaidi kupeperusha bendera ya chama chetu,” alisema Ndii.
- Papa aitangaza leo kuwa siku ya kufunga na kuombea Kongo, Sudan
- Diwani wa Chadema auawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga
Wachambuzi wa siasa za nchi hiyo wanamulika uamuzi huo na kumtaja Joshua Osih kuwa mtu anayepewa nafasi zaidi ya kugombea ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani.