Aliyekuwa mwananfunzi na kiongozi wa chuo Kikuu cha Meru, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa polisi nchini kenya.
Mwanafunzi huyo aliuawa siku ya Jumanne, katika eneo la Nchiru, Tigania West Kenya wakati wa maandamano ya wanafunzi wa chuo hiko waliokuwa wakilalamika juu ya ongezeko la ada dhidi ya Chuo hiko.
Kufuatia kifo hiko cha Mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini Kenya kimezua shutuma mpya za mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na maafisa polisi nchini humo.
Vyombo vya habari nchini Kenya vimemnukuu shuhuda mmoja akisema polisi walimkimbiza Evans wakamfikia kisha mmoja wao akampiga risasi na kuondoka.
Mkuu wa polisi Jenerali Joseph Boinnet ameamuru kufanyika uchunguzi kuhusu kifo hicho baada ya kuwepo kwa wanasiasa na makundi ya wanaharakati waliokuwa wakitaka mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na polisi kukoma mara moja.
-
Watalii wakatazwa kutoka kimahusiano na wazawa
-
Watuhumiwa 10 chini ya ulinzi kufuatia Diwani aliyeuawa kwa mapanga
Shirika huru la kiraia linalofuatilia shughuli za polisi (IPOA) limesema limewatuma maafisa wake kuchunguza tukio hilo.
Ipoa wamesema maafisa wa uchunguzi wametukwa kwa lengo la: “kuchunguza kuhusu yaliyotokea wakati wa mauaji hayo na iwapo kuna mtu anayefaa kulaumiwa, na kuhakikisha afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na hatia anawajibishwa kisheria.”
Wakenya mtandaoni wamekuwa wakishutumu mauaji hayo,