Kipa wa Sudan, Akram El Hadi ameiokowa timu yake ya taifa baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penalti wakati timu yake ilipoishinida Libya na kuibuka nafasi ya tatu katika mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Afrika (CHAN.
Awali Akram alishindwa kuihimili krosi kutoka kwa Salem Ablo iliochangia sare hiyo kwa Libya zikiwa zimesalia dakika sita tu kwa mechi kuisha
Aidha, Katika awamu ya mikwaju ya penalti , Sudan ilifanikiwa kusukuma mikwaju yote minne ndani huku mikwaju ya Elmehdi Elhouni na Ablo wa Libya ikizuiwa na Akram.
Hata hivyo, Ni shaba ya pili kwa Sudan katika fainali za mshindani hayo ya CHAN baada ya kuibuka tena nafasi ya tatu walipokuwa waandalizi wa mashndano hayo mnamo 2011, huku Libya wakiibuka mabingwa miaka mitatu baada ya hapo.