Kipa wa zamani wa Chelsea,  Mark Schwarzer, amesema kuwa mlinda mlango namba moja wa Manchester United, David de Gea amekuwa akionyesha uwezo wa kawaida tofauti na zamani.

Schwarzer amesema kuwa mabao mengi anayofungwa yanatokana na makosa yake binafsi.

“Mabao mengi anayofungwa yametokana na makosa yake binafsi, makosa aliyofanya kipindi hicho ni mengi kuliko aliyofanya miaka sita au saba, iliyopita,” alisema Schwarzer .

Schwarzer amesema De Gea alikubali kufungwa kwa uzembe kwenye michezo ya Ligi Kuu England wakati United ilipocheza dhidi ya Crystal Palace na Southampton.

De Gea ambaye amesaini mkataba mpya ndani ya United utakaodumu mpaka 2023, amekuwa akibebeshwa lawama kwa kufanya makosa yanayopelekea timu yake kufungwa.

Hivi karibuni mlinda mlango huyo mashuhuri wa mashetani wekundu alisaini mkataba mpya ambao unamuwezesha kubaki Old Trafford hadi mwaka 2023 huku akilipwa mshahara wa Paundi 500,000 kwa juma.

Misri yapata kocha mpya
Video: Mkuu wa mkoa Mororgoro katika tanuru la moto, Mjadala mzito kura polisi kabla uchaguzi