Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia mwalimu wa shule ya sekondari Kate Wilayani Nkasi, Peter Salamba kwa kumpiga kwa fimbo usoni mwanafunzi wa kidato cha tatu, Nicholous kwimba (17) wakati akiwadhibu kwa kuchelewa kuwasili shuleni asubuhi na kumsababishia upofu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Mathias Nyange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mei 21, mwaka huu saa mbili na nusu asubuhi wakati mtuhumiwa alipowaadhibu mwanafunzi huyo kwa kosa la kuchelewa kuwasili shuleni hapo.

“Hata hivyo, mkasa huu pamoja na kutokea tangu Mei, mwaka huu walimu shuleni hapo waliuficha kwa kutotoa taarifa ya kweli ili kumlinda mtuhumiwa, wakidai kuwa mwanafunzi huyo alijeruhiwa macho yote mawili wakati akikata mti” kamanda ameeleza.

Pia amewapongeza raia wema ambao waliwataarifu askari polisi kuhusu tukio hilo na kusababisha mtuhumiwa akamatwe na kuhojiwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, Dk. John Lawi ameliambia mtanzania kuwa mwanafunzi huyo amepokelewa na kulazwa katika wodi namba tatu kitanda namba sita kwa matibabu.

“Kitabibu kwa sasa ni mapema mno kusema kuwa amepofuka isipokuwa tumemweka katika uangalinzi wa kitabibu kwa siku tano ambapo majibu sahihi ya kitabibu yataainisha wazi kama amepofuka au la” ameeleza Dk. Lawi.

Kwa upannde wake mwanafunzi Nicholaus ameeleza kuwa mwalimu huyo alimchapa viboko viwili makalioni na fimbo ya tatu alimpiga usoni na kumsababishia maumivu makali machoni na hapo hapo hakuweza kuona tena.

Aidha baba yake mzazi, Cresia Kwimba amesema kuwa anachotaka ni mwalimu huyo aliyemjeruhi mwanae asifikishwe mahakamani, bali achangie matibabu ya kumuuguza mwanaye.

 

 

 

 

Kisa cha ferooz, Luludiva kuwasaidia wahudumu wa baa
Mbaroni kwa kukutwa na mafuta ya maiti ya binadamu