Waziri wa afya nchini Uganda, amezindua kipimo binafsi cha Virusi vya Ukimwi kwa kutumia mdomo lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi kupima afya zao hususani wanaume.

Uzinduzi huo umelenga kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi ifikapo 2020.

Kifaa hicho kimetengenezwa na ‘ Orasure technologies’ mahususi kwa vijana wadogo kuanzia umri wa miaka 18 hadi 24, na kundi lililo katika hatari kubwa ya maambukizi ya Ukimwi, kundi la wafanyabiashara ya ngono.

” kwasasa tunawalenga sana vijana wadogo kuanzia mika 18 hadi 24 ambao wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, lakini pia tutawapa wanawake vifaa hivi kwaajili ya wenza wao, pia tutawapa wanaofanya biashara ya ngono” amesema Geofrey Tasi afisa wa kitengo cha upimaji Ukimwi.

Kifaa hicho hakihusishi damu wakati wa upimaji, kinahitaji mate pekee ambayo kama mtu ameathirika na virusi vya Ukimwi yanakuwa na tishu ambazo kifaa cha kupimia kitazisoma.

Kwamujibu wa takwimu zilizotolewa na taasisi ya Ukimwi Uganda (UAC), zinaonesha kuwa kila wiki kuna maambukizi mapya ya watu 1000 na kila mwakwa watu 23,000 hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

 

Mtalii afariki parashuti ilopogoma kufunguka akiruka mlima Kilimanjaro
Video:Zahera alichelewa, hana mshambuliaji, atengeneze Yanga mpya