Baraza la Michezo la Taifa ‘BMT’ limetangaza kuanza cha mchakato wa Uchaguzi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), utakaofanyika Mei 13, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ofisa wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Najaha Bakari, ametaja nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Rais na Makamu wake, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

Najaha amesema anapaswa kuwa Mtanzania, amehitimu elimu ya msingi na kuendelea, ajue kusoma na kuandika, asiwe na historia ya kukutwa na hatia ya kesi ya jinai au kufungwa.

“Yoyote mwenye sifa kwa mujibu wa katiba ya TPBRC anashauriwa kujitokeza kuchukua fomu,” alisema.

Najaha amesema ada ya fomu ya kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais, Katibu na Mweka Hazina wa Shirikisho hilo ni shilingi 100,000 wakati ada ya kugombea ujumbe ni shilingi 50,000.

Young Africans yarejea kambini, kuondoka kesho
PICHA: JK akutana na wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo mjini Boston, MarekaniPICHA: