Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limekutana kwa ajili ya kuwasilisha na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya kata zake mbalimbali.

Katika kikao hicho cha kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo ameipongeza Kishapu kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu (CAG).

Butondo amewataka madiwani waendelee kushikamana na kuwahudumia wananchi katika kata zao ili kueleta maendeleo katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Aidha, amesema kuwa ni wajibu wao kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo katika kata zao sambamba na kuendelea kuwahamasisha kuhusu kilimo hususani cha mazao yanayostahimili ukame.

“Waheshimiwa tuwahudumie wananchi katika kata zetu na hasa ukizingatia hivi sasa Serikali inapiganaia katika kufufua zao la pamba katika wilaya yetu nasi tuwahamasishe kulima,” alisema.

Hata hivyo, ameongeza kuwa katika kikao hicho Baraza linajipima wapi wamefikia katika miradi ya maendeleo na wapi wamekwama hivyo kuweza kutatua changamoto hizo na hatimaye kusonga mbele.

Serikali yazionya kampuni za usambazaji pembejeo
Video: Ndugai awasha moto maadili kwa wabunge, 34 kunyongwa