Wabunge wastaafu kwa tiketi ya CHADEMA, Esther Matiko, Ester Bulaya na Halima Mdee wamepita kwa kishindo kwenye kura za maoni walipoomba ridhaa ya kugombea tena ubunge kupitia chama hicho.

Esther Matiko ameibuka mshindi katika Jimbo la Tarime Mjini akipata kura 80 ambazo ni sawa na 97. 6%, alikuwa mgombea pekee na alihitaji kura za Ndio au Hapana ambapo amepata Ndio 80 (97.6) na Hapana 2 (2.4%).

Kura 126 za Ndiyo zimempa ushindi Ester Bulaya kwenye kura za maoni katika Jimbo la Bunda Mjini ambapo alikuwa mgombea pekee kwenye kura hizo hivyo alihitaji kura za Ndio au Hapana. Kura zilizopigwa ni 128, za Ndio ni 126 na Hapana 2.

Halima Mdee ameshinda kura za maoni kwa jimbo la Kawe kwa kura 63 (71.5%) akifuatiwa na Doricus Mwilafi mwenye kura 13 (14.7%), Joel Mwakalebela kura 7 (7.9%) na Felsta Njau kura 5 (5.6%)

CAS wamuibua Guardiola, ataka kuombwa radhi
Wassira achukua fomu Bunda, Lugola arudi Mwibara