Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson ameshinda nafasi ya urais wa Umoja wa Mabunge Duniani – IPU, kwenye Uchaguzi uliofanyika Jijini Luanda, nchini Angola.
Wawakilishi 700 kutoka nchi 130 walikutana jijini Luanda nchini humo, kwa ajili ya uchaguzi huo ambapo alishiriki na kuomba kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja huo kwenye mdahalo wa uchaguzi wakati Mkutano huowa 147.
Katika maelezo yake, Dkt. Tulia aliwaeleza Wajumbe wa Mkutano huo kuwa, endapo watamchagua atahakikisha anasimamia misingi ya Umoja huo kwa kuongeza Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Oktoba, 2023.
Uchaguzi huo, uliwapa fursa Wanawake wanne kutoka nchi ya Senegal, Somalia, Malawi na Tanzania kugombea nafasi hiyo, ambapo hatua hiyo inaifanya Tanzania kuendelea kuaminika katika medani za siasa kote ulimwenguni.