Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans Tuisila Kisinda ameanza  mazoezi chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo, baada ya kupona majeraha ya bega yaliyokuwa yakimkabili.

Kiungo huyo kutoka DR Congo aliumia wakati wa mchezo wa Gwambina FC ambao ulimalizika kwa Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja, mwezi uliopita.

Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa Kisinda ameanza  mazoezi chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo  kutokana na majeraha ya bega yaliyokuwa yakimkabili.

Bumbuli ameongeza kuwa Kisinda alifanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine tangu Jumapili na jana Jumatatu hivyo anaendelea vizuri.

“Kwa sasa Kisinda yupo vizuri, alianza mzoezi tangu Jumapili na jana jumatatu alifanya mazoezi na wenzake, lakini suala la kucheza mchezo wa Mei 08 litaendelea kubaki kwa wahusika wa benchi la ufundi kwa sababu wao ndio wanafahamu mipango na mikakati kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC.” Amesema Bumbuli

Wachezaji wengine wenye majeraha ndani ya kikois cha Young Africans ni Lamine Moro pamoja na Dickson Job ambao nao hali zao zinaendelea vizuri  wakati Carlinhos kwa upande wake amepelekwa Hospitali kwa matibabu zaidi.

Carlinhons alipatwa na majeraha ya paja kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho, wakati Young Africans ilipocheza dhidi ya Tanzania Prisons juma lililopitra mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mahakama yamwachia huru aliyekuwa mgombea Ubunge Bukoba mjini
Coastal Union: Mgunda hajafukuzwa