Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya RS Berkane ya Morocco, Twisila Kisinda amesema bado kikosi chao kina nafasi ya kuendeleza ubabe dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kama walivyofanya mwishoni mwa juma lililopita (April 27).
Simba SC ilikubali kupoteza ugenini kwa kuchapwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane, mchezo uliounguruma mjini Berkane ncnhini Morocco, matokeo yaliyoifanya klabu hiyo ya Msimbazi kubaki na alama nne katika msimamo wa Kundi D.
Kisinda ambaye alisajiliwa na RS Berkane mwanzoni mwa msimu huu akitokea Young Africans, amesema haamini kucheza na Simba SC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huenda ikawa sababu ya kupoteza, kama ilivyozoeleka kwa wageni wengi wanapokua Uwanjani hapo.
“Malengo yetu safari hii ni kuweza kufika mbali katika michuano hii, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika kila mchezo uliosalia ili tuweze kutimiza malengo yetu.”
“Sisi kucheza katika Uwanja wa Mkapa siamini basi itakuwa asilimia zote kwamba Simba SC watashinda mchezo huo, tunahitaji kupata matokeo mazuri tukiwa kwao japo wamekuwa na historia nzuri wakiwa katika uwanja wao,” ame Kisinda
Mara ya mwisho Simba SC ilipocheza Uwanja wa Benjamin Mkapa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa Kundi D, Kombe la Shirikisho BArani Afrika.