Kisiwa kikubwa cha utalii cha Hawaii kimekumbwa na kimbunga kinachotajwa kuwa kikali chenye kipimo cha ritcha 6.8 kilichotajwa kuanzia kwenye mlima wa volcano uitwao Kilauea.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tetemeko hilo liliambatana na upepo mkali ambao uliharibu mkubwa wa makazi ya watu na miundombinu ya umeme na maji na kuwafanya watu kuondoka majumbani mwao.
”Tunaishi eneo la mashambani Leilani, karibu vitalu sita vilisambaratishiwa mbali na mlipuko tuliondolewa eneo hilo saa kadhaa zilizopita na sasa tumejihifadhi kwa marafiki. Nusu saa baada ya kimbunga hicho , nilishangaa kukuta mitandao mingi imeandika juu ya tukio hilo, kwa hiyo mimi na binti yangu tukatoka kwenda kujionea kwa macho yetu kwakweli unaweza kusikia na kuhisi mlipuko ukiwa umbali wa nusu maili na kadiri unavyokaribia eneo la tukio ndivyo unavyozidi kulihisi. Ilikuwa kama wakati mtu anavyopiga gitaa la besi kwakweli nzito, na unaweza kuhisi kweli nguvu ya uji wa volkano, rangi nayo sasa ilikuwa ya kustaajabisha na sauti ya volkano hiyo kwakweli ni maajabu makubwa” amesema shuhuda Maija Stenback.
Hata hivyo baadhi ya watu wamegoma kuhama katika makazi hayo Kufuatia hali hiyo ya hatari ambapo wakazi wapatao 1,700 wamehamishwa kutoka eneo hilo na tayari vituo vya kijamii vimefunguliwa ili kutoa makazi kwa waathirika.
Maafisa wa serikali wameendelea kutoa angalizo kwa wakazi wa maeneo hayo na ya jirani kwamba kwa wiki ijayo yote wanapaswa kuwa katika tahadhari kubwa na mara wakihisi viashiria vya kutaka kulipuka kwa volkano haraka iwezekanavyo na hii ni kwa wale wote waliogoma kuyahama makazi yao
Aidha Gavana wa Hawaii , David Ige amesema kuwa alikuwa ametoa ushawishi kwa wanajeshi na vikosi vya usalama wa taifa hilo kusaidia katika shughuli za uokozi wa maelfu ya watu.
Kilauea ni mojawapo ya eneo lenye volkano yenye nguvu na mlipuko zaidi duniani kufuatia mfululizo wa matetemeko ya hivi karibuni.