Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Real Madrid ya Hispania Eden Hazard, anatafanyiwa upasuaji mwingine kwenye mguu wa kulia, ambao utamuweka nje ya dimba kwa mwezi moja.
Hazard aliumia mguu wa kulia Machi 2020, na tangu wakati huo amekua sio mwenye furaha kutokana na jeraha hili, hivyo imeonekana kuna ulazima wa kufanyiwa kupasuaji ili kumaliza tatizo linalomsumbua.
Kuwa nje kwa mwezi mmoja kutamfanya aukose mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kati ya kikosi cha Real Madrid ambacho kitacheza dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa robo fainali mwezi ujao.
“Kwa siku kadhaa zijazo, mchezaji wetu Eden Hazard, atafanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia,” taarifa ya klabu hiyo imeeleza.
Hazard amecheza michezo 22 tu msimu huu huku akianza kwenye michezo minane ya LaLiga wakati akifunga bao moja na kusaidia kupatikana mawili, pia hajafanikiwa kucheza tena tangu alipoingia kwenye mchezo dhidi ya Alaves Februari 19, mwaka huu.